• HABARI MPYA

  Wednesday, March 01, 2023

  WAZIRI MKUU AAGIZA UKARABATI UWANJA WA MKAPA UHARAKISHWE


  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kuanza haraka ukarabati wa Uwanja wa Mpira wa Miguu wa Benjamin Mkapa ili ukidhi mahitaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika CAF baada ya kuufanyia ukaguzi hivi karibuni.
  Ametoa agizo hilo leo (Jumatano, Machi 1, 2023) jijini Dar es Salaam alipotembelea kukagua hali ya uwanja huo baada CAF kutaka ufanyiwe marekebisho katika baadhi ya maeneo 
  “Ili mradi CAF wametupa onyo, ni onyo ambalo wametupa na muda wa kufanya marekebisho na muda huo waliotupa ni lazima tuanze jambo ndipo waridhie mambo mengine yaendelee, nimekuja kuwaambia msiruhusu uwanja huu umefungwa na CAF na kuzipeleka timu zetu zikacheze ugenini”.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WAZIRI MKUU AAGIZA UKARABATI UWANJA WA MKAPA UHARAKISHWE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top