• HABARI MPYA

  Thursday, August 05, 2021

  VAN GAAL AREJESHWA KUFUNDISHA TIMU YA TAIFA YA UHOLANZI

  KOCHA Louis van Gaal ameteuliwa kuwa kufundisha timu ya taifa ya Uholanzi kwa mara ya tatu kufuatia timu hiyo kufanya vibaya kwenye Euro, akichukua nafasi ya Frank de Boer.
  De Boer alijiuzulu ukocha wa Uholanzi baada ya kipigo cha 2-0 kutoka kwa Jamhuri ya Czech Hatua ya 16 Bora Euro 2020.
  Kocha huyo mwenye umri wa miaka 69 aliifundisha “Oranje” kuanzia 2000-2002, timu hiyo iliposhindwa kufuzu Kombe la Dunia.
  Lakini alipata mafanikio zaidi awamu ya pili alipoiwezesha kushika nafasi ya tatu katika Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil.
  Van Gaal anayekumbukwa zaidi kwa kuipa Ajax taji la Ligi ya Mabingwa mwaka 1995, pia amekochi Barcelona, Manchester United na Bayern Munich.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: VAN GAAL AREJESHWA KUFUNDISHA TIMU YA TAIFA YA UHOLANZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top