• HABARI MPYA

  Thursday, August 05, 2021

  ASTON VILLA YAMSAJILI LEON BAILEY KWA PAUNI MILIONI 30

  KLABU ya Aston Villa imemsajili mshambuliaji Leon Bailey kutoka Bayer Leverkusen kwa ada ya Pauni Milioni 30.
  Mjamaica huyo mwenye umri wa miaka 23 alifunga mabao 15 na assists 11  kwenye mashindano yote akiwa na Leverkusen aliyojiunga nayo Januari 2017 kutoka Genk ya Ubelgiji.
  Na Aston Villa inamchukua nyota huyo akazibe pengo la Jack Grealish anayeuzwa kwa dau la Pauni Milioni 100 kwenda Manchester City.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ASTON VILLA YAMSAJILI LEON BAILEY KWA PAUNI MILIONI 30 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top