• HABARI MPYA

  Thursday, August 05, 2021

  MJAMAICA ASHINDA MBIO ZA KURUKA VIHUNZI MITA 110 OLIMPIKI

  MJAMAICA Hansle Parchment ameshinda Medali ya Dhahabu katika mbio za kuruka vihunzi mita 110 akimpiku Mmarekani, Grant Holloway hatua za mwishoni baada ya kutumia muda wa sekunde 13.04.
  Holloway, bingwa wa dunia, alikuwa anaongoza hadi baada ya vihunzi tisa kati ya 10, lakini bahati mbaya akaishiwa nguvu mwishoni na Parchment akampita na kwenda kuchukua Dhahabu baada ya kuondoka na Shaba kwenye Michezo ya London mwaka 2012.
  Pedro Pichardo, kinara wa dunia kwenye outdoors mwaka 2021, ameshinda Medali ya Dhahabu kwenye kuruka, Mreno huyo akiweka rekodi ya umbali wa mita 17.98.

  Mchina, Zhu Yaming akaondoka na Fedha na Hugues Fabrice Zango akachukua Shaba akiipa Medali ya kwanza kabisa nchi yake, Burkina Faso Medali kwenye Olympiki. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MJAMAICA ASHINDA MBIO ZA KURUKA VIHUNZI MITA 110 OLIMPIKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top