• HABARI MPYA

  Sunday, August 01, 2021

  ELAINE THOMPSON-HERAH AVUNJA REKODI RIADHA MITA 100

  MJAMAICA Elaine Thompson-Herah amevunja rekodi ya Florence Griffith Joyner mwenye umri wa miaka 33 kwenye mbio za mita 100 wanawake katika michezo ya Olimpiki inayoendelea Jijini Tokyo, Japan.
  Elaine ametumia muda wa sekunde 10.61 kutetea taji lake na kuiongoza Jamaica kuendelea kukusanya Medali, akivunja rekodi ya Joyner aliyemaliza kwa sekunde 10.62 kwenye Olimpiki ya mwaka 1988, Seoul.
  Thompson-Herah amemshinda mpinzani wake, Shelly-Ann Fraser-Pryce kwa sekunde 13, wakati Shericka Jackson ameshinda Medali ya Shaba.   • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ELAINE THOMPSON-HERAH AVUNJA REKODI RIADHA MITA 100 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top