• HABARI MPYA

  Thursday, August 05, 2021

  AZAM FC YATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA KAGAME BAADA YA KUICHAPA LA MESSAGER NGOZI YA BURUNDI 1-0 CHAMAZI
  WENYEJI, Azam FC wamefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki ns Kati, maarufu kama CECAFA Kagame Cup baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Le Messager Ngonzi ya Burundi jioni ya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Bao pekee la Azam FC leo limefungwa na winga wake, Iddi Kipagwile aliyerejea Chamazi baada ya msimu mmoja wa kucheza kwa mkopo Namungo FC ya Lindi dakika ya 22 akimalizia krosi ya chinichini ya Tepsi Evance.
  Azam FC inafikisha pointi sita baada ya mechi mbili na inatangulia Nusu Fainali, ikifuatiwa na mabingwa watetezi, KCCA wenye pointi tatu baada ya kuifunga KMKM 1-0 leo.
  KMKM na Le Messager Ngozi zinabaki na pointi zao moja kila moja kuelekea mechi za mwisho Jumamosi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA KAGAME BAADA YA KUICHAPA LA MESSAGER NGOZI YA BURUNDI 1-0 CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top