• HABARI MPYA

  Sunday, August 01, 2021

  MHESHIMIWA RAIS SAMIAH AIPONGEZA TIMU YA VIJANA KWA KUTWAA UBINGWA WA CECAFA CHALLENGE U23 ETHIOPIA


  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samiah Suluhu Hassan ameipongeza timu ya vijana kwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati kwa vijana chini ya umri wa miaka 23, CECAFA Challenge U23.
  Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Rais Samia ameandika; "Nawapongeza timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 23 kwa kutwaa ubingwa wa Mashindano ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA-2021),".
  Mheshimiwa Rais amesema ushindi hui ni heshima kwa nchi na ni chachu ya kukuza michezo Tanzania. 
  "Natoa wito kwa wadau wa michezo kuendeleza jitihada za kukuza michezo yetu," amesema.


  Timu ya Tanzania ilitwaa ubingwa wa CECAFA Challenge U23 juzi baada ya kuifunga Burundi kwa penalti 6-5 kufuatia sare ya 0-0 ndani ya dakika 90 Uwanja wa Bahir Dar Jijini Bahir Dar nchini Ethiopia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MHESHIMIWA RAIS SAMIAH AIPONGEZA TIMU YA VIJANA KWA KUTWAA UBINGWA WA CECAFA CHALLENGE U23 ETHIOPIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top