• HABARI MPYA

  Sunday, August 01, 2021

  YANGA SC YAANZA NA SARE YA 1-1 KOMBE LA KAGAME IKIWA PUNGUFU DHIDI YA BIG BULLET YA MALAWI


  WENYEJI, Yanga SC wamelazimishwa sare ya 1-1 na Nyasa Big Bullet ya Malawi katika mchezo wa ufunguzi wa Kundi A Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Yanga ilitangulia kwa bao la mshambuliaji Waziri Junior dakika ya nane kwa kichwa akimalizia krosi ya mchezaji mpya, Dickson Ambundo kutoka Dodoma Jiji FC.
  Na Nyasa Big Bullet wakasawazisha dakika ya 
  30 kwa penalti ya Chiukepo Msowoya kufuatia beki Abdallah Shaibu 'Ninja' kumchezea vibaya Mnigeria, Babatunde Aderpoje.
  Yanga SC ilimaliza pungufu baada ya kipa wake, Ramadhan Awam Kabwili kutolewa kwa kadi nyekundu kufuatia kumuangusha Hassan Kajoke kwenye boksi dakika ya 89.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YAANZA NA SARE YA 1-1 KOMBE LA KAGAME IKIWA PUNGUFU DHIDI YA BIG BULLET YA MALAWI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top