• HABARI MPYA

  Thursday, August 05, 2021

  MESSI KUONDOKA BARCELONA BAADA YA KUSHINDWANA NAO

  MWANASOKA bora wa zamani wa dunia, Lionel Messi ataondoka Barcelona dirisha hili licha ya awali kutarajiwa kwa kiasi kikubwa kubaki Nou Camp.
  Messi amekuwa mchezaji huru tangu mwezi uliopita baada ya mkataba wake kumalizika ingawa alitarajiwa kubaki Barca kutokana na mazungumzo yaliyokuwa yanaendelea vizuri baina ya pande zote mbili.
  Messi alitarajiwa kubaki kwa punguzo la malipo ya mshahara kwa mkataba wa muda mrefu, lakini vigogo hao wa Katalunya wamethibitisha makubaliano yamekufa kwa sababu za kiuchumi na misingi za La Liga Hispania.


  Messi amekuwa akihusishwa na kuhamia klabu za Manchester City na Paris Saint Germain na maendeleo ya ghafla yameibuka juu ya mipango hiyo baada ya kukutana na mchezaji mwenzake wa zamani Barcelona ambaye pia ni rafiki yake wa karibu, Mbrazil Neymar.
  Neymar aliondoka Barca kuhamia PSG mwaka 2017 na alisema anatamani kucheza tena pamoja na Muargentina huyo siku moja.
  Jumatano Neymar aliweka picha kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamiii ikimuonyesha akiwa na Messi pamoja na wachezaji wengine watatu wa PSG, Angel Di Maria, Leo Parades na Marco Veratti, aliyoiandikia maelezo: 'amigos.'
  Picha hiyo sasa imeibua tetesi kwamba Messi sasa yuko njiani kuhamia PSG na kwa sababu mkataba wake umeisha Nou Camp  hakuna cha kumzuia tena.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MESSI KUONDOKA BARCELONA BAADA YA KUSHINDWANA NAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top