• HABARI MPYA

  Tuesday, August 03, 2021

  BINTI WA 'KITANZANIA' ASHINDA MEDALI YA DHAHABU OLIMPIKI

  BINTI Mjerumani mwenye asili ya Tanzania, Malaika Mihambo ameshinda Medali ya Dhahabu kwenye Kuruka Mbali (Long Jump) katika michezo ya Olimpiki inayoendelea Jijini Tokyo, Japan mapema leo.
  Malakia mwenye umri wa miaka 27, ameruka umbali wa mita 7 akifuatiwa na mkongwe wa Marekani, Brittney Reese aliyechukua Medali ya Fedha na Mnigeria, Ese Brume aliyeondoka na Medali ya Shaba baada ya wote kuruka umbali wa mita 6.97.
  Mihambo aliyeshinda ubingwa wa dunia mwaka 2019 na kushika nafasi ya nne Olimpiki ya 2016 – anazaliwa na mama Mjrumani na baba Mtanzania.
  Kwa ushindi huo, Malaika kwa sasa ndiye bingwa wa Olimpiki, Ulaya na Dunia katika Long Jump.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BINTI WA 'KITANZANIA' ASHINDA MEDALI YA DHAHABU OLIMPIKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top