• HABARI MPYA

  Monday, August 02, 2021

  AZAM FC YAANZA VYEMA KOMBE LA KAGAME BAADA YA KUWACHAPA MABINGWA WATETEZI, KCCA YA UGANDA 2-0 CHAMAZI

   TIMU ya Azam FC imeanza vyema michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya mabingwa watetezi, KCCA ya Uganda usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Mabao ya Azam FC katika mchezo huo wa Kundi B yamefungwa na mshambuliaji Paul Peter ambaye amerejea Chamazi baada ya msimu mmoja wa kucheza kwa mkopo KMC ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
  Mechi nyingine ya kundi hilo leo, KMKM ya Zanzibar imelazimishwa sare ya 1-1 na Le Messager Ngonzi ya Burundi, wakati mchezo wa Kundi A, Express ya Uganda imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Atlabara ya Sudan Kusini hapo Azam Complex.


  Azam sasa inaongoza Kundi B ikifuatiwa na Messager na KMKM zenye pointi moja kila moja, wakati KCCA inashika mkia haina pointi, wakati Kundi A Express inaongoza ikifuatiwa na Nyasa Big Bullet ya Malawi na Yanga ya Dar es Salaam zenye pointi moja kila moja na Atlabara inashika mkia haina pointi.
  Kesho ni mapumziko na keshokutwa Express itamenyana na Big Bullet na Yanga na Atlabara Uwanja wa Benjamin Mkapa mechi za Kundi A.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAANZA VYEMA KOMBE LA KAGAME BAADA YA KUWACHAPA MABINGWA WATETEZI, KCCA YA UGANDA 2-0 CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top