• HABARI MPYA

  Thursday, August 05, 2021

  MWANARIADHA WA BELARUS OLIMPIKI AWASILI SALAM POLAND

  MWANARIADHA wa Belarus kwenye Olimpiki, Krystsina Tsimanouskaya, aliyekataa kurejea nchini kwake kwa kuhofia usalama wake baada ya kutofautiana na viongozi wake wa timu ya Olimpiki amewasili Warsaw jana usiku ambako atapewa hifadhi.
  Binti huyo alipewa visa ya kibindam kufuatia kuondoka kwenye Michezo ya Tokyo baada ya kukwepa kurejeshwa kwao na viongozi wake kufuatia kukaidi agizo la makocha wake kukimbia mbio za wanne wanne mita 400 akisema hajawahi kukimbia kabla.
  Kwa mujibu wa video iliyopostiwa na Waziri Mkuu, Mateusz Morawiecki binti huyo alionekana katika Jiji hilo la Poland akiwa na viongozi mbalimbali.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MWANARIADHA WA BELARUS OLIMPIKI AWASILI SALAM POLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top