• HABARI MPYA

  Jumatano, Agosti 12, 2020

  PAMBANO LA MIKE TYSON NA ROY JONES JR. LASOGEZWA MBELE

  PAMBANO la bingwa wa zamani wa ngumi uzito wa juu, Mike Tyson dhidi ya Roy Jones Jr. limesogezwa mbele hadi Novemba 28.
  Tyson mwenye umri wa miaka 54, ambaye alitawala ndondi za uzito wa juu kwa takriban miaka 20 ybaada ya kutwaa taji la dunia mwaka 1987, alitarajiwa kupigana na mpinzani wa umri wa miaka 51- Jones katika pambano la Raundi la Nane Jijini California Septemba 12.
  Gwiji huyo na bingwa wa dunia asiyepingika wa uzito wa juu enzi hizo, Tyson atarejea ulingoni baada ya miaka 15 tangu astaafu.
  Pambano la Mike Tyson dhidi ya Roy Jones Jr. limesogezwa mbele hadi Novemba 28 PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Jones alipigana kwa mara ya mwisho mwaka 2018 wakati Tyson mara ya mwisho alipanda ulingoni miaka 15 iliyopita alipopigwa na Kevin McBride.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: PAMBANO LA MIKE TYSON NA ROY JONES JR. LASOGEZWA MBELE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top