• HABARI MPYA

  Jumapili, Agosti 02, 2020

  NYOTA WA COASTAL UNION, AYOUB LYANGA ATUA AZAM FC KWA MKATABA WA MIAKA MIWILI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIUNGO mshambuliaji, Ayoub Lyanga, amekamilisha taratibu za kujiunga na Azam FC, baada ya kusaini mkataba rasmi wa miaka miwili akitokea Coastal Union kwa usajili huru.
  Lyanga amesaini mkataba huo mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin 'Popat', mara baada ya kufuzu vipimo vya afya.
  Nyota huyo amekuwa kwenye kiwango kizuri msimu huu akiisaidia vilivyo Coastal, akifunga jumla ya mabao nane kwenye ligi na kuchangia pasi nane zilizozaa mabao.
  Lyanga anakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na Azam FC kwenye dirisha hili la usajili, baada ya awali kuwanasa viungo Awesu Awesu, Ally Niyonzima.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NYOTA WA COASTAL UNION, AYOUB LYANGA ATUA AZAM FC KWA MKATABA WA MIAKA MIWILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top