• HABARI MPYA

    Saturday, August 01, 2020

    IHEFU YAPANDA LIGI KUU BAADA YA KUISHUSHA MBAO FC KIRUMBA, MBEYA CTY YANUSURIKA SOKONE

    Na Mwandishi Wetu, MWANZA
    TIMU ya Ihefu FC ya Mbarali mkoani Mbeya imefanikiwa kupanda Ligi Kuu ya Tanzania Bara licha ya kufungwa 4-2 na wenyeji, Mbao FC kwenye mchezo wa Mchujo (Play-Off) uliofanyika Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
    Matokeo hayo yanamaanisha Ihefu inapanda kwa mabao ya ugenini baada ya ushindi wa 2-0 Alhamisi kwenye mchezo wa kwanza Uwanja wa Highland Estate huko Mbarali kufanya sare ya jumla ya 4-4.  
    Mabao ya Mbao FC leo yamefungwa na Waziri Junior dakika ya nane na 45 na ushei, Michael Masinda aliyejifunga dakika ya 47 na Datus Peter kwa penalti dakika ya 90 na ushei, wakati ya Ihefu yamefungwa na Willy Mgaya na Geoffrey Kinyozi. 


    Nayo Mbeya City imefanikwa kubaki Ligi Kuu baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Geita Gold ya Geita, bao pekee la Geoffrey Manyasi aliyejifunga kipindo cha kwanza.
    Mbeya City inabaki Ligi Kuu kwa ushindi wa jumla wa 2-1 baada ya sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza Uwanja wa sekondari ya Nayankungu, Geita Alhamisi.
    Hii maana yake, msimu ujao Jiji la Mbeya litakuwa na timu tatu katika Ligi Kuu – mbali na Ihefu FC na Mbeya City, nyingine ni Tanzana Prisons. 

    Mbeya City na Mbao FC ziliangukia katika mechi za Play-Offs baada ya kushika nafasi za 15 na 16 kwenye Ligi Kuu, wakati Ihefu na Geita zilishika nafasi za pili kwenye makundi A na B ya Ligi Daraja la Kwanza.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: IHEFU YAPANDA LIGI KUU BAADA YA KUISHUSHA MBAO FC KIRUMBA, MBEYA CTY YANUSURIKA SOKONE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top