• HABARI MPYA

  Jumapili, Agosti 09, 2020

  BARCELONA YATINGA ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA

  Lionel Messi akishangilia na wenzake baada ya kuifungia Barcelona bao la pili dakika ya 23 katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Napoli kwenye mchezo wa marudiano Hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Camp Nou. Mabao mengine ya Barcelona yalifungwa na Clement Lenglet dakika ya 10 na Luis Suarez kwa penalti dakika ya 45 na ushei, wakati la Napoli lilifungwa na Lorenzo Insigne dakika ya 45 na ushei kwa penalti pia na sasa Barca inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 4-2 kufuatia sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza na itamenyana na Bayern Munich katika Robo Fainali 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BARCELONA YATINGA ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top