• HABARI MPYA

  Jumamosi, Agosti 01, 2020

  AZAM FC YAMSAJILI KIUNGO WA KIMATAIFA WA RWANDA ALLY NIYONZIMA KUTOKA RAYON SPORT

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Azam FC imekamilisha usajili wa kiungo mkabaji wa kimataifa wa Rwanda, Ally Niyonzima, kwa mkataba wa miaka miwili.
  Niyonzima aliyekuwa akicheza Rayon Sports ya Rwanda, usajili wake ni sehemu ya mapendekezo ya benchi la ufundi la Azam FC chini ya Kocha Mkuu, Mromania Aristica Cioaba.
  Kiungo huyo nyota mwenye umbo kubwa, amesaini mkataba leo Jumamosi mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin 'Popat'.
  Niyonzima, ambaye yumo kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Rwanda, 'Amavubi', anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa Azam FC kwa ajili ya msimu ujao baada ya kiungo mwingine, mzawa Awesu Awesu kutoka Kagera Sugar ya Bukoba.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM FC YAMSAJILI KIUNGO WA KIMATAIFA WA RWANDA ALLY NIYONZIMA KUTOKA RAYON SPORT Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top