• HABARI MPYA

  Ijumaa, Agosti 14, 2020

  AZAM FC NAYO YAJA NA TAMASHA LA WIKI YA CHAMAZI LITAKALOFANYIKA KUANZIA JUMAPILI HADI AGOSTI 23 DAR

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Azam FC tunawaletea tamasha kubwa la Azam FC Festival, kwa ajili ya kujiweka karibu na mashabiki hususani wakazi wa Chamazi inapotokea timu hii.
  Uzinduzi wa wiki ya tamasha hilo 'Wiki ya Chamazi', unatarajia kufanyika keshokutwa Jumapili saa 4.00 asubuhi na kilele chake  kitakuwa Agosti 23 mwaka huu.
  Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Azam FC, Thabith Zakaria 'Zaka Zakazi' amesea kwamba tamasha la Azam FC Festival litakuwa la wiki moja kuanzia keshokutwa Jumapili hadi siku ya kilele chake, Agosti 23 mwaka huu.
  "Tumeandaa tamasha linaloitwa Azam FC Festival, tamasha hili ni maalumu kwa ajili ya klabu na mashabiki wake, hasa mashabiki waliopo Chamazi na mashabiki waliopo Temeke lakini na wengine wote kutoka sehemu yoyote ile ambayo wanaweza kufika katika eneo lile (Azam Complex)."
  Baadhi ya mambo yatakayofanyika siku ya uzinduzi, ni mbio za vikundi vya Jogging vya eneo hilo, zitakazoanzia Mzambarauni hadi Mbande kabla ya kufanyika uzinduzi rasmi saa 4 asubuhi uwanjani Azam Complex.
  Aidha kwenye uzinduzi huo kutakuwa na mashindano maalumu ya  timu za waandishi wa habari za michezo, watakashindana kuwania ubingwa.
  Wiki ya Chamazi itaendelea Jumatatu ijayo, kwa kuanza michuano rasmi ya wakazi wa Kata Chamazi, itakayohusisha timu tano za mitaa tisa ya kata hiyo dhidi ya nyingine zitakazoalikwa, michuano itakayohitimika siku ya kilele cha tamasha hilo kwa mchezo wa fainali.
  Siku ya kileleni cha 'Azam FC Festival', Agosti 23 mwaka huu, mbali na kuwa na burudani kibao ndani ya viunga vya Azam Complex, pia timu hii itatumia siku hiyo kucheza mchezo rasmi wa kirafiki na timu moja ya nje ya nchi kwa ajili ya kutambulisha kikosi cha msimu ujao pamoja na jezi.
  Vilevile kabla ya mechi hiyo kubwa, miongoni mwa mechi ya utangulizi, itakuwa ni ile fainali ya mashindano ya wakazi wa Chamazi pamoja na mechi za timu za vijana za Azam FC.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM FC NAYO YAJA NA TAMASHA LA WIKI YA CHAMAZI LITAKALOFANYIKA KUANZIA JUMAPILI HADI AGOSTI 23 DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top