• HABARI MPYA

  Ijumaa, Februari 07, 2020

  SAMATTA AENDA KUJIFUA KIVYAKE DUBAI BAADA YA KUPEWA MAPUMZIKO MAFUPI ASTON VILLA

  Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta akinywa maji baada ya mazoezi makali gym jana Dubai. Samatta yupo Dubai akitumia kipindi cha mapumziko mafupi ya klabu yake katika Ligi Kuu ya England kujifua binafsi kujiweka fiti zaidi ili aweze kumudu mikiki ya ligi hiyo.

  Baada ya kufunga kwenye mechi yake ya kwanza EPL mwishoni kwa wiki iliyopta, Aston Villa ikichapwa 2-1 na wenyeji, AFC Bournemouth Uwanja wa Vitality akina Samatta hawatakuwa na mchezo mwingine hadi Jumapili ijayo, watakapoikaribisha Tottenham Hotspur.
  Kazi na dawa; Hapa Mbwana Samatta akicheza kwenye ngamia baada ya mazoezi
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SAMATTA AENDA KUJIFUA KIVYAKE DUBAI BAADA YA KUPEWA MAPUMZIKO MAFUPI ASTON VILLA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top