• HABARI MPYA

  Saturday, July 27, 2019

  COSTA APIGA MABAO NNE ATLETICO YAICHAPA REAL MADRID 7-3

  Mshambuliaji Diego Costa akishangilia baada ya kuifungia Atletico Madrid mabao manne dakika ya kwanza, 28, 45 kwa penalti na 51 katika ushindi wa 7-3 dhidi ya mahasimu wao, Real Madrid kwenye mchezo wa kirafiki wa kujiandaa na msimu mpya usiku wa kuamkia leo Uwanja wa MetLife mjini East Rutherford, New Jersey, New York, Marekani. Mabao mengine ya Atletico Madrid yalifungwa na Joao Felix dakika ya nane, Ángel Martin Correa dakika ya 19 na Vitolo dakika ya 70, wakati ya Real Madrid yamefungwa na Nacho dakika ya 59, Karim Benzema kwa penalti dakika ya 85 na Javi Hernandez dakika ya 89. Lakini Costa hakumaliza mchezo baada ya kutolewa dakika ya 65 kwa pamoja na Carvajal baada ya wawili hao kugombana 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: COSTA APIGA MABAO NNE ATLETICO YAICHAPA REAL MADRID 7-3 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top