• HABARI MPYA

  Monday, July 22, 2019

  SIMBA QUEENS YACHEZA MECHI MBILI MFULULIZO SIKU MOJA, YASHINDA NA KUTOA SARE

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Simba Queens jana imecheza mechi mbili za kujipima nguvu katika ziara yake ya nchini Ujerumani na kushinda moja na kutoa sare moja.
  Kwa mujibu wa Mratibu wa Simba Queens, Suleiman Makanya mechi za jana zilikuwa ni dhidi ya timu za St Pauli.
  Makanya mechi alisema ya kwanza walicheza na timu B ya St Pauli B na kushinda 3-1 wakati ya pili walicheza na timu A ya St Pauli na kutoka sare ya 2-2.

  Nahodha wa Simba Queens akipokea msaada wa jezi baada ya mechi na St Pauli

  Wachezaji wa Simba Queens katika picha ya pamoja na St Pauli

  Mabao yote ya Simba Queens yalifungwa Amina Ramadhani mawili kwenye mechi ya kwanza moja mechi ya pili na Mwanahamisi Omar ‘Gaucho’ moja katika kila mechi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA QUEENS YACHEZA MECHI MBILI MFULULIZO SIKU MOJA, YASHINDA NA KUTOA SARE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top