• HABARI MPYA

  Friday, July 12, 2019

  YANGA SC KUMENYANA NA AS VITA AGOSTI 4 TAIFA KATIKA KILELE CHA SIKU YA MWANANCHI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Yanga itamenyana na vigogo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), AS Vita katika mchezo wa kirafiki Agosti 4, Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
  Mchezo huo utafanyika katika kilele cha Wiki Mwanachi, tamasha maalum la kutambulisha kikosi kipya cha klabu pamoja na jezi za msimu.
  Makamu Mwenyekiti wa Yanga SC, Frederick Mwakalebela amesema kwamba Wiki Mwanachi itaanza Julai 28 na kufikia kilele Agosti 4 na kuwakuw ana mchezo wa kirafiki dhidi ya AS Vita.
  “Mbali na masuala ya kijamii ambayo yametengenezewa utaratibu na ratiba itakayosambazwa katika matawi yote ya klabu nchi nzima na groups zote za whatsap za Yanga, kadhalika na vyomba vya habari,”.

  Mwakalebela amesema kwamba baada ya uzinduzi rasmi itafuata shoo kabambe ya mtaa kwa mtaa lengo ni kukusanya idadi kubwa ya wananchi.
  “Wana Yanga wajiandae kwa burudani kutoka wa wasanii, waimbaji, waigizaji, pamoja na zawadi kemkem katika kusanya kusanya kusanya hii, hakika haijwahi tokea katika historia ya mpira nchini mwetu na pengine kungineko,”amesema Katibu huyo wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania (FFF).
  Mwakalebela amezitaja shughuli mbali mbali zitakazofanyika katika Wiki ya Mwananchi ni pamoja na Kufanya Usafi, Kupanda Maua na Miti, Matembezi ya Mshikamano na Kuzuru kaburi la Hayati Mzee Karume katika (Kusanya Kijiji Roadshow), Kutembelea Hospitali ya Ocean Road na kutoa msaada wa vitu na mahitaji mbalimbali kwa wagonjwa wenye uhitaji.
  “Kupanda Miti kiwanja cha Yanga, Kigamboni na Kusanya kijiji Kigamboni Kutembelea Vituo Vya Watoto Yatima na kuchangia damu hospitali Uzinduzi wa Matawi Mapya ya Yanga DSM na Mikoani,”amesema.
  Kwa sasa kikosi cha Yanga SC kipo kambini mjini Morogoro chini ya Kaimu Kocha Mkuu, Msambia Noel Mwandila kikijiandaa na msimu mpya na Kocha Mkuu, Mkongo Mwinyi Zahera anatarajiwa kuwa amewasili hadi mapema wiki ijayo. 
  Wachezaji wanaotarajiwa kuchezea Yanga msimu ujao ni makipa; Farouk Shikalo, Metacha Mnata, Ramadhani Kabwili na Klaus Kindoki. 
  Mabeki; Paul Godfrey ‘Boxer’, Juma Abdul, Muharami Issa ‘Marcelo’, Jaffary Mohamed, Andrew Vincent ‘Dante’, Kelvin Yondani, Ally Ally, Mustafa Suleiman, Ally Mtoni ‘Sonso’ na Lamine Moro.
  Viungo; Papy Kabamba Tshishimbi, Feisal Salum ‘Fei Toto’, Mohamed Issa ‘Banka’, Patrick Sibomana, Issa Bigirimana, Mapinduzi Balama, Mrisho Ngassa, Deus Kaseke, Raphael Daud Loth na Abdulaziz Makame ‘Bui’.
  Washambuliaji; Sadney Khoetage, Juma Balinya na Kalengo Maybin.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC KUMENYANA NA AS VITA AGOSTI 4 TAIFA KATIKA KILELE CHA SIKU YA MWANANCHI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top