• HABARI MPYA

  Tuesday, July 23, 2019

  YANGA WAWE MAKINI, WASIKUBALI KUZUNGUKWA NA WANAOZUNGUKA

  Na Dominick Salamba, DAR ES SALAAM
  SIKU moja niliwahi kupita mahali fulani na kukutana na hadithi moja nzuri ya ufahamu lakini mbaya kimatokeo,Iliwahusu jamaa watatu ambao walikuwa wanamshinikiza mzazi wao mmoja aliyebaki ambaye ni mama yao kuwa anatakiwa kutoa idhini ili nyumba na eneo lao lililobakia mikononi mwao kwa uangalizi wa mama yao liuzwe na wagawane kila mtu na chake,lakini mama huyo alikataa juu ya hilo hivyo watoto wale waliamua kumuwekea sumu ambayo ilikadiriwa kuchukua siku 20 hadi 30 kuweza kuleta umauti kwa binadamu ambaye ataitumia,walifanikiwa na mama alianza kuugua taratibu na wao wakijifanya kama hawajui kitu na kuanza kuwataarifu majirani na watu mbalimbali juu ya kuugua huko kwa mama yao na kwenda mbali zaidi kuomba misaada ya pesa ya matibabu na chakula pia pindi walipopata hizo pesa hawakununua dawa wala chakula zaidi walitumia kwa mambo yao binafsi huku mama yao akizidi kudhohofu,kwa mwonekano wa nje walijifanya wenye huzuni kuu na huruma kubwa kumbe ulikuwa ndiyo mpango wao ili watimize lililo lao tu peke yao,hawakuwaza mama yao sio wao peke yao,ana baba yake,mama yake,kaka,dada,jamaa na rafiki zake hivyo kwa dhambi ya mali na uroho uliopitiliza hawakujali wala kuwaza yote zaidi waligubikwa na roho ya ukatili tamaa na kiu ya mali ambazo pengine zikuwa faraja kwa wengi.
  Niliache hilo kwani mwishowe litaniliza na kujikuta nashindwa kufikisha ujumbe nilioukusudia.
  Kwanza nianze kuwapongeza viongozi wa YANGA waliochaguliwa nadhani nitakuwa ndiyo wa mwisho kutoa pongezi tena za kuchelewa lakini nilikuwa nafikiria cha kuandika toka wamechaguliwa na leo ndiyo nimekipata sasa,hakuna asiyejua Yanga SC ilivyopitia msimu uliopita na ile dhana ya damu nzito ilitimia pale wanachama,wadau na wapenzi wa timu hiyo walipoamua kuisaidia timu hadi ilifanikiwa kumaliza ligi katika nafasi ya pili na leo tunapoongea timu imepata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa ngazi ya klabu bingwa barani Afrika.
  Wakati timu inapitia vipindi vigumu kiasi kile na wengi wakiuzunishwa sana juu ya hali ile mimi nilikua najiuliza hivi ni kweli Yanga pamoja na yote yaliyopo kweli walitakiwa kufikia pale lakini ghafla nikawa nawaza kuna pesa za udhamini wa Sportpesa,pesa za udhamini wa matangazo ya runinga,makusanyo wa viwanjani ingawa hayakuwa kwa kiasi kikubwa,lakini kubwa kuliko ni miongoni mwa timu ambazo zilitumia jezi nyingi msimu uliopita na sidhani kama hazikuwa sehemu ya klabu kwani zilikuwa na nembo na kutumika pia na timu sasa kama ndivyo ina maana zilikuwa zinauzwa na timu haipati kitu?niliwaza na kukosa majibu ya hili nikaona nitulie pia.
  Uongozi mpya umepatikana na kwa bahati nzuri viongozi wakaomba makundi yavunjwe na kuungana na mpira uchezwe na timu iwe moja na madhaifu yote ya nyuma yabaki kama historia na kuyatumia kupatia uzoefu kwa miaka ijayo na wananchi wakaunga mkono na kuendelea kuisapoti timu kwa hali na mali,haraka kamati zikaundwa kamati ya mashindano na uchumi,mipango na fedha uku kukiundwa pia kamati ya hamasa ambayo nakiri imefanya mambo makubwa sana na kurudisha hali na Hamasa kwa mashabiki na wapenzi wa soka yanga ikaenda kwenye kubwa kuliko ilikuwa ya kihistoria watu wakajitoa pesa zikachangwa kwa kiwango kikubwa wadau wakubwa wawili Rostam Aziz na GSM wakatia pesa sio pesa tu bali pesa ya maana.
  Tena wakaenda mbali na kuahidi kuzidi kuisaidia Yanga katika kufikia malengo kubwa ili jina la timu liendane na hali ya uchumi wa klabu hiyo kongwe hapa nchini.na kweli timu ikaanza kusajili mapema kabisa ndani ya nchi na nje ya nchi wachezaji mahiri na vijana tena wenye vipaji hasa na bado mambo yakazidi kunoga kukatangazwa wiki ya Mwananchi ambayo ingeenda kufungua ukurasa mpya kwa timu na wanamichezo pia kubwa zaidi tena kampuni ya GSM ikashinda zabuni ya kusambaza vifaa vya michezo kwa timu ya Yanga SC  hasa hasa niliguswa na kusambaza jezi za Yanga SC nikaona neema nyingine katika mpira wetu kwani hakuna asiyejua nguvu ya kibiashara ya GSM siyo ndani ya nchi tu hapana bali Afrika nzima ni kampuni kubwa ambayo inaubora wa aina yake na kuamika pia hivyo yanga wamepata dodo wanasema watoto wa mjini.
  Na hii ikanifanya nikumbuke zile jezi kama njugu zilizokuwa zikuzwa na wasiojulikana kuona sasa ndio mwisho na kufikiria zaidi namna ambavyo watalipokea hili hasa hofu yangu ikinipeleka kwenye mivutano ya ndani na kuweza kuleta migogoro tu ili mambo yakwame.
  Nisiingie ndani sana huko ila wanayanga ambao ni sehemu ya watanzania wengi wapenda michezo ambao wananafasi ya kuleta maendeleo kupitia mchezo wa soka ambao sasa ni biashara kubwa duniani kuwa sasa kama timu mnapitia njia safi kwenda kwenye maendeleo makubwa ya klabu yenu kuna watu wenye weledi ambao wameamua kuitoa Yanga ilipo ili isonge mbele zaidi ila kuna kundi dogo la watu wabinafsi na waroho ambao hawa hawawezi kukoma hata mwisho wa dunia wao ni watu wa kupinga na kupanga mbinu chafu mahala popote penye heri na mafanikio wakiona wao wametupwa nje ya mfumo na mara nyingi utumia akili kubwa katika ndogo kufanikisha malengo yao msikubali wawagawe pigeni hatua unganeni wakataeni kwa ushawishi wao wa hovyo wakishindwa kwenu wataingia kwa wachezaji na benchi la ufundi kujaribu kuharibu nako huko ili tu mambo yawe hovyo na mrudi nyuma mlikotoka ili wao wapige pesa tena kipindi hiki hapana msikubali.
  Watendelea kuwashawishi kwa hoja dhaifu na za hovyo juu ya  maendeleo ya kweli ili tu mgawanyike na kuwarudisha nyuma msikubali na hakikisheni mnawalinda wachezaji wenu na kuwafanya wawe wamoja wasitumike na genge la wahuni na endapo mtagundua waonyeni na wakikaidi watoeni kwenye kundi mmeamua kwenda mbele kweli nendeni.
  Hivi leo kuna mtu anaweza kuhoji uwezo wa kibiashara wa GSM?kampuni ambayo ni kubwa na italeta makubwa kwa maana ya mapato na kuinua thamani ya klabu.Nafikiri mnatakiwa kuwatengenezea mazingira mazuri ya kibiashara wawekezaji kama hawa na wengine kwa maslahi mapana ya timu yenu,hakuna asiyejua dunia ya sasa inaelekea wapi kisoka na ushindani ni mkubwa sana ambapo nguvu ya kipesa ndio imeshika mpira wa kileo.
  Mwisho nitoe rai yangu kwa uongozi wa klabu ya Yanga mmepewa dhamana kubwa sana kwani wanachama wamewaamini hivyo msikubali kutikiswa na makundi madogo kemeheni na ikibidi fichueni makundi hayo ili taifa litambue maadaui wa maendeleo ya waliowengi kwani mpira ni ajira na ni chanzo cha kuchangia pato la Taifa wakati taifa likielekea kwenye uchumi wa kati.

  (Mwandishi wa makala haya, Dominick Salamba unaweza kumfollow Instagram @dominicksalamba  au kuwasiliana naye kwa simu nambari +255713942770)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA WAWE MAKINI, WASIKUBALI KUZUNGUKWA NA WANAOZUNGUKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top