• HABARI MPYA

  Saturday, July 13, 2019

  LIPULI FC YAMSAJILI BEKI WA MBAO FC KUZIBA PENGO LA ALLY SONSO ALIYEHAMIA YANGA

  Na Mwandishi Wetu, IRINGA
  KLABU ya Lipuli FC ya Iringa, maarufu kama ‘Wana Paluhengo’ imejiimarisha kwa kumsajili beki wa kati wa Mbao FC ya Mwanza, David Mwasa Majige.
  Rais wa Lipuli FC, Mama Jesca Msambatavangu ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online kwamba Mwasa amesaini mkataba wa mwaka mmoja kujiunga na washindi wa pili wa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
  Na mchezaji huyo anajiunga na Lipuli FC iliyofungwa 1-0 na Azam FC katika fainali ya Kombe la TFF, maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) kwenda kuziba pengo la Ally Mtoni ‘Sonso’ aliyehamia kwa vigogo wan chi, Yanga SC.

  Rais wa Lipuli FC, Mama Jesca Msambatavangu (kushoto) akimtambulisha David Mwasa baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja

  Pamoja na kumsajili Mwasa, Mama Jesca pia amesema wamefanikiwa kumuongezea mkataba wa mwaka mmoja, mshambuliaji wao mahiri, Paul Nonga aliyeafunga mabao saba msimu uliopita wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
  Na tayari Lipuli FC imemuajiri kocha Mrundi, Harerimana Huruma kutoka nchini Burundi ambaye atakuwa anasaidiwa na Samuel Moja, kufuatia kuondoka kwa Suleiman Abdallah Matola aliyejiunga na Polisi Tanzania iliyopanda Ligi Kuu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIPULI FC YAMSAJILI BEKI WA MBAO FC KUZIBA PENGO LA ALLY SONSO ALIYEHAMIA YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top