• HABARI MPYA

  Jumatano, Julai 10, 2019

  KAGERA SUGAR YAENDELEA KUIMARISHA KIKOSI KWA KUMSAJILI MSHAMBULIAJI KUTOKA DRC

  Na Mwandishi Wetu, BUKOBA
  TIMU ya Kagera Sugar ya Bukoba imeendelea kujiimarisha baada ya kusajili wachezaji wawili wapya, akiwemo nyota wa klabu ya Bakavu Dawa FC ya Jamhuri ya Kodemokrasia ya Kongo (DRC), Jackson Kibirige.
  Pamoja na mchezaji huyo wa timu ya taifa ya vijana ya Uganda chini ya umari wa miaka 23, Kagera Sugar inayofundishwa na kocha mzawa Meciky Mexime imemsajili Abdul Swamadu Kassim kutoka Malindi FC ya Zanzibar
  Kibirige anakuwa mchezaji wa pili mpya wa kigeni kusajiliwa na Kagera Sugar baada ya kiungo mkabaji Moussa Hadji Mosi aliyejiunga na na timu hiyo kutoka Leslierres ya Ligi Kuu ya kwao, Burundi.

  Jackson Kibirige (kushoto) akisaini mkataba wa kujiunga na Kagera Sugar kutoka Bakavu Dawa FC ya DRC 

  Na Kwa ujumla Kibirige anakuwa mchezaji wa mpya 10 kujiunga na timu hyo pamoja na Mosi, wengine ni Yussuph Mhilu kutoka Yanga SC aliyecheza kwa mkopo Ndanda FC msimu uliopita, Zawadi Mauya kutoka Lipuli FC, Ally Shomari kutoka Mtibwa Sugar, Abdallah Seseme kutoka Mwadui FC, Awesu Ally Awesu kutoka Singida United, Erick Kyaruzi, Frank Ikobela, wote kutoka Mbeya City ya Mbeya na  Evarist Mjwahuki kutoka Mbao FC ya Mwanza.
  Kagera Sugar imepania kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu ujao baada ya kunusurika kushuka Daraja msimu uliopita.
  Ikumbukwe Kagera Sugar na Mwadui FC zilinusurika kushuka daraja baada ya kubaki Ligi Kuu ya Tanzania Bara kupitia mechi zao Play-Off dhidi ya Pamba SC na Geita Gold Mine za Daraja la Kwanza. 
  Mabao ya Ally Ramadhani dakika ya 51 na Japhet Makalayi dakika ya 59 yaliipa Kagera Sugar ushindi wa 2-0 dhidi ya Pamba SC Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba Juni 9 baada ya timu hizo kutoka sare ya kwenye mchezo wa kwanza Juni 3 Uwanja wa Nyamagana mjini Mwanza.
  Na hiyo ni baada ya Kagera Sugar kumaliza nafasi ya 18 katika Ligi Kuu, nyuma ya Mwadui FC iliyomaliza nafasi ya 17 ambayo iliitoa Geita Gold katika mechi ya mchujo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KAGERA SUGAR YAENDELEA KUIMARISHA KIKOSI KWA KUMSAJILI MSHAMBULIAJI KUTOKA DRC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top