• HABARI MPYA

  Tuesday, July 30, 2019

  YANGA SC YAENDELEZA UBABE MECHI ZA KUJIPIMA NGUVU MORO, YAICHAPA 2-0 FRIENDS RANGERS

  Na Mwandishi Wetu, MOROGORO
  YANGA SC leo imeendeleza wimbi la ushindi katika mechi zake za kujipima nguvu kwenye kambi yake Morogoro kujiandaa na msimu mpya baada kuichapa Friends Rangers ya daraja la Kwanza mabao 2-0 Uwanja wa Chuo cha Biblia, Bigwa.
  Mabao ya Yanga SC katika mchezo wa leo yamefungwa na mshambuliaji wake mpya kutoka Namibia, Sadney Urikhob dakika ya 38 na Nahodha mpya, kiungo Papy Kabamba Tshishimbi raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) dakika ya 64.
  Yanga SC itateremka tena dimbani Jumapili wiki hii kumenyana na Kariobangi Sharks ya Kenya Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam katika kilele cha Wiki ya Mwananchi.

  Mechi nne zilizotangulia Yanga imeshinda 10-1 dhidi ya dhidi ya Tanzanite, 7-0 dhidi ya ATN, 2-0 dhidi ya Moro Kids na 1-0 dhidi ya Mawenzi Market.
  Na yote hayo ni maandalizi ya mchezo wao wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Yanga SC wakianza na Township Rollers ya Botswana kati ya Agosti 9 na 11 mjini Dar es Salaam kabla ya kurudiana nao mjini Gaborone kati ya Agosti 23 na 25.
  Ikifanikiwa kuvuka raundi ya kwanza Yanga itakutana na mshindi kati ya Green Mamba ya Eswatini na Zesco ya Zambia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YAENDELEZA UBABE MECHI ZA KUJIPIMA NGUVU MORO, YAICHAPA 2-0 FRIENDS RANGERS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top