• HABARI MPYA

  Jumapili, Julai 21, 2019

  YANGA SC ILIPOZINDUA JEZI MPYA KWA KUIPIGA SIMBA 1-0 TAIFA 1992

  KIKOSI cha Yanga SC kilichowafunga watani wao wa jadi, Simba SC 1-0,  katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Aprili 12, mwaka 1992 Uwanja wa Taifa (sasa Uhuru) mjimi Dar es Salaam, bao pekee la Nahodha wake, beki wa kushoto Kenneth Pius Mkapa dakika ya 10. Yanga SC walikuwa wanavaa jezi hizo kwa mara ya kwanza siku hiyo baada ya kupewa zawadi nchini Misri na mashabiki wao Wazungu. Waliosimama kutoka kulia ni Meneja Charles Mgombelo, Salum Kabunda ‘Ninja’ (marehemu), Mathod Mogella (marehemu), Abeid Mziba, David Mwakalebela, Hamisi Gaga (marehemu), Kenny Mkapa na kocha Syllersaid Mziray (marehemu). 
  Waliochuchumaa kutoka kulia ni Godwin Aswile, Justin Mtekere (marehemu)., Steven Nemes, Thomas Kipese na Said Mwamba ‘Kizota’ (marehemu).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA SC ILIPOZINDUA JEZI MPYA KWA KUIPIGA SIMBA 1-0 TAIFA 1992 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top