• HABARI MPYA

  Jumanne, Julai 23, 2019

  MTIBWA SUGAR YAMREJESHA SAID MOHAMMED NDUDA NA KUSAINI WENGINE WAPYA WAWILI

  Na Mwandishi Wetu, MOROGORO
  KIPA Said Mohammed Nduda amesaini mkataba wa kujiunga tena na klabu ya Mtibwa Sugar misimu miwii tangu aondoke kuhamia kwa vigogo, Simba SC ya Dar es Salaam.
  Nduda ni kati ya wachezaji wapya watatu wapya waliosajiliwa Mtibwa Sugar hadi sasa, wengine ni beki wa kushoto, Mohamed Abdallah Rashid kutoka Singida United na kiungo mshambuliaji Awadh Salum Juma kutoka African Lyon.
  Ndunda amerejea Mtibwa Sugar baada ya misimu miwili ya kuwa na Simba, ambayo aliimalizia kwa kucheza kwa mkopo kwa nusu msimu Ndanda FC ya Mtwara.
  Mohamed amewahi kuzitumikia timu za taifa chini ya miaka 17, 20 na sasa anaitumikia timu ya taifa chini ya miaka 23 sawa na Awadh.
  Wakati Ndunda anasajiliwa, Mtibwa Sugar imeondokewa na wachezaji watatu tayari, kipa Benedicto Tinocco aliyejiunga na Kagera Sugar ya Bukoba, beki Nickson Kibabage aliyejiunga na Difaa Hassan El-Jadidi ya Morocco na kiungo Rodgers Gabriel aliyejiunga na Mwadui FC.
  Wakati huo huo: Mtibwa Sugar itakuwa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Aigle Noir ya Burundi Jumamosi Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR YAMREJESHA SAID MOHAMMED NDUDA NA KUSAINI WENGINE WAPYA WAWILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top