• HABARI MPYA

    Friday, July 19, 2019

    YANGA SC YAENDELEZA WIMBI LA USHINDI MECHI ZA KAMBINI, YAIPIGA MORO KIDS 2-0

    Na Mwandishi Wetu, MOROGORO
    TIMU ya Yanga SC imeshinda mechi ya pili mfululizo leo katika kambi yake ya Morogoro kujiandaa na msimu upya baada ya kuichapa Moro Kids 2-0 Uwanja wa Chuo cha Biblia, Bigwa mkoani Morogoro.
    Mshambuliaji mpya, Juma Balinya kutoka Uganda leo amefunga bao lake la pili tangu ajiunge na timu hiyo baada ya kufunga pia kwenye ushindi wa 10-1 dhidi ya Tanzanites mwanzoni mwa wiki.
    Balinya aliyesajiliwa kutoka Polisi FC ya Uganda leo amefunga bao la kwanza kwa penalti wakati bao la pili limefungwa na beki, Paul Godfrey ‘Boxer’, yote kipindi cha kwanza.
    Juma Balinya amefunga bao lake la pili leo Yanga SC tangu awasili mwezi huu kutoka Polisi ya kwao, Uganda 

    Katika mchezo dhidi ya Tanzanite, nyota wa mchezo wa alikuwa ni kiungo mshambuliaji, Mrisho Khalfan Ngassa aliyefunga mabao matatu peke yake dhidi ya timu hiyo ya Daraja la Pili.
    Mabao mengine yalifungwa na Feisal Salum, Raphael Daudi, Mapinduzi Balama, Mkongo Papy Kabamba Tshishimbi, Wanyarwanda Patrick Sibomana, Issa Bigirimana, Mganda Juma Balinya, 
    Yanga itamenyana na vigogo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), AS Vita katika mchezo wa kirafiki Agosti 4, Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
    Mchezo huo utafanyika katika kilele cha Wiki Mwanachi, tamasha maalum la kutambulisha kikosi kipya cha klabu pamoja na jezi za msimu.
    Kwa sasa kikosi cha Yanga SC kipo kambini mjini Morogoro chini ya Kaimu Kocha Mkuu, Msambia Noel Mwandila kikijiandaa na msimu mpya na Kocha Mkuu, Mkongo Mwinyi Zahera anatarajiwa kuwa amewasili hadi mapema wiki ijayo. 
    Wachezaji wanaotarajiwa kuchezea Yanga msimu ujao ni makipa; Farouk Shikalo, Metacha Mnata, Ramadhani Kabwili na Klaus Kindoki. 
    Mabeki; Paul Godfrey ‘Boxer’, Juma Abdul, Muharami Issa ‘Marcelo’, Jaffary Mohamed, Andrew Vincent ‘Dante’, Kelvin Yondani, Ally Ally, Mustafa Suleiman, Ally Mtoni ‘Sonso’ na Lamine Moro.
    Viungo; Papy Kabamba Tshishimbi, Said Juma ‘Makapu’, Feisal Salum ‘Fei Toto’, Mohamed Issa ‘Banka’, Patrick Sibomana, Issa Bigirimana, Mapinduzi Balama, Mrisho Ngassa, Deus Kaseke, Raphael Daud Loth na Abdulaziz Makame ‘Bui’.
    Washambuliaji; Sadney Urikhob, Juma Balinya na Kalengo Maybin.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC YAENDELEZA WIMBI LA USHINDI MECHI ZA KAMBINI, YAIPIGA MORO KIDS 2-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top