• HABARI MPYA

  Jumamosi, Julai 20, 2019

  ALGERIA YATAWALA TUZO ZA AFCON 2019, SENEGAL WAUNGWANA ZAIDI

  PAMOJA na kutwaa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kwa mara ya pili katika historia yao, Algeria pia wametawala kwenye tuzo binafsi.
  Kiungo Ismael Bennacer amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mashindano baada ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 21 kutoa mchango mkubwa kwenye kikosi kilichoshinda taji la pili tu baada ya lile la mwaka 1990.
  Kipa Rais M’Bolhi anayechukuliwa kama bora zaidi Afrika, alishinda tuzo mbili juzi, kwanza Mlinda Mlango Bora wa Mashindano na Mchezaji Bora wa Mechi.
  Kiungo wa Algeria, Ismael Bennacer amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mashindano 

  Kwa upande mwingine, mshambuliaji wa Nigeria, Odion Ighalo amekuwa mfungaji bora wa mashindano kufuatia kufunga mabao matano kwenye michuano hiyo.
  Senegal iliambulia tuzo moja baada ya kiungo wake, Krepin Diatta kuchaguliwa Mchezaji Bora Chipukizi wa Mashindano huku kikosi cha Simba wa Teranga kikishinda tuzo ta Soka ya Kiungwana.
  WASHINDI WA TUZO ZOTE
  Mchezaji Bora wa Mashindano: Ismael Bennacer (Algeria)
  Kipa Bora: Rais M’Bolhi (Algeria)
  Mfungaji Bora: Odion Jude Ighalo (Nigeria, mabao matano)
  Mchezaji Bora Chipukizi: Krepin Diatta (Senegal)
  Soka ya Kiungwana]: Senegal
  KIKOSI CHA KOMBAINI YA MASHINDANO
  Kipa: Rais M’Bolhi (Algeria)
  Mabeki: Lamine Gassama (Senegal), Yassine Meriah (Tunisia), Youssouf Sabaly (Senegal), Kalidou Koulibaly (Senegal),
  Viungo: Adlene Guediora (Algeria), Idrissa Gana Gueye (Senegal), Ismael Bennacer (Algeria)
  Washambuliaji: Riyad Mahrez (Algeria), Sadio Mane (Senegal), Odion Jude Ighalo (Nigeria)
  Kocha: Djamel Belmadi (Algeria)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ALGERIA YATAWALA TUZO ZA AFCON 2019, SENEGAL WAUNGWANA ZAIDI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top