• HABARI MPYA

  Thursday, July 18, 2019

  NIGERIA YAMALIZA NAFASI YA TATU AFCON BAADA YA KUWAPIGA 1-0 TUNSIA

  TIMU ya taifa ya Nigeria ‘Super Eagles’ imefanikiwa kumaliza nafasi ya tatu katika Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Tunisia leo.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee Uwanja wa Al Salam mjini Cairo nchini Misri, mshambuliaji wa Shanghai Shenhua ya China, Odion Jude Ighalo dakika ya tatu ya mchezo huo.
  Nigeria iliangukia kwenye mchezo wa kusaka nafasi ya tatu baada ya kufungwa 2-1 na Algeria katika mchezo wa Nusu Fainali.

  Tunisia nayo iliangukia kwenye mchezo huo wa kuwania nafasi ya tatu baada ya kuhapwa bao 1-0 na Senegal katika Nusu Fainali.
  Na fainali ya AFCON 2019 itafuatia Ijumaa Saa 4:00 usiku pia baina ya Senegal na Algeria Uwanja wa Kimataifa wa Cairo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NIGERIA YAMALIZA NAFASI YA TATU AFCON BAADA YA KUWAPIGA 1-0 TUNSIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top