• HABARI MPYA

  Sunday, July 14, 2019

  SIMBA SC YA MWAKA 2004 ILIKUWA YA MOTO MOTO, YANGA WALIKOMA

  Kikosi cha Simba SC mwaka 2004 kutoka kulia waliosimama; Victor Costa, Suleiman Matola, Primus Kasonso, Said Swedi, Christopher Alex (marehemu), Amri Said na Meneja Innocent Njovu. Waliochuchumaa kutoka kulia ni Athumani Machuppa, Shaaban Kisiga, Juma Kaseja, Ulimboka Mwakingwe, Soud Abdallah ‘Carlos’ na Haruna Moshi ‘Boban’. Kikosi hiki kiliwafunga watani, Yanga mechi za mwaka huo, ya kwanza 2-1 Agosti 7 na ya pili 1-0 Septemba 18.
  Agosti 7 mabao ya Simba yalifungwa na  Shaaban Kisiga ‘Malobe’ dakika ya 64 na Ulimboka Mwakingwe dakika ya 76 huku la Yanga likifungwa na Mkongo, Pitchou Kongo dakika ya 48 na Septemba 18 ushindi wa 1-0 ulitokana na bao pekee la Athumani Machuppa dakika ya 82.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YA MWAKA 2004 ILIKUWA YA MOTO MOTO, YANGA WALIKOMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top