• HABARI MPYA

  Jumatano, Julai 24, 2019

  SERIKALI YAMZUIA MO DEWJI KUMILIKI ASILIMIA 49 ZA HISA PEKE YAKE SIMBA SC

  Na Asha Said, DAR ES SALAAM            
  WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amesema mfumo wa uwekezaji katika klabu za Tanzania ni Hisa asilimia 49 kwa wawekezaji na hisa  Asilimia 51 kwa wanachama. 
  Akizungumza na Waandishi wa Habari leo mjini Dar es Salaam leo, Waziri Mwakyembe amesema kwamba ikiwa Asilimia 49 za wawekezaji lazima kuwa na wawekezaji kuanzia watatu.
  Waziri Mwakyembe amesema kwamba hairuhusiwi kwa mwekezaji mmoja pekee kuhodhi asilimia 49 za hisa za klabu.

  Waziri amesema wakati mchakato ulipoanza aliwaambia TFF wasimamie hilo lakini hawakufanya hivyo kwa sababu Uwekezaji wa klabu ya Simba hisa asilimia 49 zinamilikiwa na Mohammed ‘Mo’ Dewji.
  Amesema sasa Serikali imeanza mchakato wa kurekebisha kanuni za uwekezaji kwenye klabu za Tanzania na ameongeza kwa sasa mchakato huo utasimamiwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na si Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) tena.
  Amesema itaundwa Kamati ndogo ya kushugulikia mchakato huo upya ikiwa na Mjumbe kutoka BMT, TFF, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Soko la Mitaji, Wadau na Mkurungezi  wa Michezo.
  Wakati Mwakyembe akizungumzia hilo, aliyewahi kuwa mdhamini wa klabu hiyo Hamisi Kilomoni, kesho atazungumza na Waandishi wa Habari kuhusu msimamo wake baada ya kauli ya Waziri huyo mwenye dhamana ya michezo hapa nchini. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SERIKALI YAMZUIA MO DEWJI KUMILIKI ASILIMIA 49 ZA HISA PEKE YAKE SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top