• HABARI MPYA

  Tuesday, July 23, 2019

  MWAMBUSI ATAKA MECHI MBILI ZA KUJIPIMA MBEYA CITY KABLA YA KUIVAA TANZANIA PRISONS

  Na Asha Said, DAR ES SALAAM                      
  KOCHA Mkuu wa timu ya Mbeya City, Juma Mwambusi, amesema anahitaji mechi nne za kirafiki kabla ya kuvaana na wapinzani timu ya Prisons, katika kuanza msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2019/20.              
  Mwambusi amesema anatambua ugumu wa mchezo huo na wapinzani wao hao ambao kila wanapokutana Mbeya City upata kichapo toka kwa wapinzani wao hao ambao nao wapo katika mkoa huo wa Mbeya.    
  Amesema timu inatarajia kuingia kambini wiki ijayo mara baada ya yeye kuanza rasmi kazi ambapo anatarajia kuanza rasmi kazi siku ya Jumatatu ya kukinoa kikosi hicho kilichopo chini ya Manispaa ya Mbeya.
  Juma Mwambusi anahitaji mechi nne za kirafiki kabla ya kuvaana Tanzania Prisons 

  Mwambusi aliyewahi kuwa Kocha Msaidizi wa klabu za Yanga na Azam, amesema kambi yao inaweza kuwa Mbeya Mjini, au nje ya mji huo kati ya Tukuyu au Kyela lengo ni kutaka kufanya vizuri.
  "Mimi nitaanza rasmi kazi siku ya Jumatatu ambayo itakuwa Julai 29, siku chache baadae tutajua kambi yetu itakuwa wapi, lengo tuanze vizuri msimu huo mpya"asema Mwambusi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MWAMBUSI ATAKA MECHI MBILI ZA KUJIPIMA MBEYA CITY KABLA YA KUIVAA TANZANIA PRISONS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top