• HABARI MPYA

  Jumanne, Julai 09, 2019

  AZAM FC NA KMC ZOTE ZAPIGWA 1-0 MICHUANO YA KOMBE LA KAGAME LA KIGALI

  Na Mwandishi Wetu, KIGALI
  TIMU za Azam FC na KMC za Dar es Salaam zote zimepoteza mechi zao za leo za michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame kwa kufungwa 1-0 kila timu na wapinzani wao.
  Ilianza kuchapwa Azam FC 1-0 na KCCA ya Uganda katika mchezo wa Kundi B mchana Uwanja wa Huye mjini Butare, bao pekee la Anaku Sadat dakika ya 49.
  Ikafuatia KMC nayo kupigwa 1-0 na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) bao pekee la Mondeko Zatu dakika ya 61 katika mchezo wa Kundi A Uwanja wa Nyamirambo mjini Kigali.

  Kwa mabingwa watetezi, Azam FC huo ni mchezo wa kwanza wanapoteza baada ya kuanza vyema kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Mukura Victory Uwanja wa Huye Julai 7.
  KMC pia wamepoteza mchezo wa kwanza leo, kufuatia sare ya 1-1 dhidi ya Atlabara ya Sudan Kusini Julai 7 pia.
  Mechi nyingine za leo; wenyeji Rayon Sports wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Atlabara katika mchezo wa Kundi A, wakati Bandari imelazimishwa sare ya 2-2 na wenyeji wengine, Mukura Victory.
  Michuano hiyo itaendelea kesho kwa mechi za Kundi D, Port ya Djibouti dhidi ya Gor Mahia ya Kenya Uwanja wa Saa 8:00 mchana na KMKM dhidi ya Manyema Union ya DRC Uwanja wa Umuganda mjini Gisenyi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM FC NA KMC ZOTE ZAPIGWA 1-0 MICHUANO YA KOMBE LA KAGAME LA KIGALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top