• HABARI MPYA

  Jumatano, Julai 31, 2019

  SPURS YAIFUNGA MADRID, MAN UNITED YAICHAPA TIMU YA SOLSKJAER

  Na Mohamed Mshangama, TANGA
  Klabu ya Tottenham Hotspur imeingia fainali kwenye kikombe cha Audi baada ya kuifunga klabu ya Real madrid goli moja kwa bila.
  Goli pekee lilofungwa na mshambuliaji wa uingereza na mfungaji bora wa kombe la dunia 2018, Harry kane kwenye dimba la Allianz arena, liliweza kuipa tiketi ya kwenda kucheza mchezo wa fainali.
  Huku kwenye mchezo mwengine wa kombe hilo Bayern Munich waliweza kuibuka na ushindi mnono wa bao 6-1.
  Magoli yaliofungwa na Sanches (22'), 2-0 Goretzka (28'), 3-0 Müller (31'), 4-0 Coman (40'), 5-0 Müller (pen. 44'), 6-0 Müller (58') yaliweza kuipeleka bayern fainali.
  Hivyo baryern watacheza mchezo wa fainali na Tottenham.
  Manchester united wakiwa ziarani huko Norway, walipata mchezo wakujipima ubavu na Kristiansund mchezo ulio chezwa kwenye dimba la Ullevaal Stadion. 
  Goli pekee lilofungwa na kiungo wa hispania Juan Mata dakika ya 91 ndio liloleta ushindi kwenye mechi hiyo.
  Huo ni mchezo wa tano kwa manchester united katika mechi za kujiandaa na msimu mpya na kuweza kushinda mechi zote hizo tano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SPURS YAIFUNGA MADRID, MAN UNITED YAICHAPA TIMU YA SOLSKJAER Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top