• HABARI MPYA

  Jumamosi, Julai 20, 2019

  NG’ANZI ATOKEA BENCHI MINNESOTA UNITED YAPIGWA 3-0 NA ASTON VILLA MECHI YA KIRAFIKI

  Na Mwandishi Wetu, MINNESOTA
  KIUNGO chipukizi Mtanzania mwenye umri wa miaka 18, Ally Ng’anzi jana amecheza mechi yake ya kwanza kikosi cha kwanza cha Minnesota United wakifungwa 3-0 na Aston Villa ya England katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Allianz Field, Saint Paul mjini Minnesota.
  Hiyo ni baada ya kupelekwa kucheza kwa mkopo Forward Madison FC ya Ligi Daraja la Tatu nchini Marekani, ijulikanayo kama USL League One na sasa amerejea Minnesota United kwa maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu ya Marekani, MSL.
  Ng’anzi aliingia dakika ya 72 kuchukua nafasi ya Miguel Ibarra katika mchezo ambao mabao ya Aston Villa yalifungwa na Jack Grealish dakika ya 36, Henri Lansbury dakika ya 82 na Birkir Bjarnason dakika ya 86.

  Ally Ng’anzi jana amecheza mechi yake ya Minnesota United wakifungwa 3-0 na Aston Villa

  Baada ya mchezo huo, kocha wa Minnesota United Adrian Heath alisema kwamba anafikiri Ng’anzi amefanya vizuri, ingawa bado anatakiwa kuzingatia maelekezo. 
  “Nafikiri amefanya vizuri. Nafikiri amefanya jambo moja au mawili, mengine hakufanya. Alikuwa kipata mpira alitaka kuonyesha hiyo ni nafasi kubwa haswa kwake,” alisema Heath.
  Heath alisema kuna mtu "aliwatonya" (aliwaibia siri)/aliwaambia juu ya uwezekano wa kumpata Nganzi, na hatimaye akatua kwa dau poa. "Kiukweli ni kama bure,” alisema Heath.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NG’ANZI ATOKEA BENCHI MINNESOTA UNITED YAPIGWA 3-0 NA ASTON VILLA MECHI YA KIRAFIKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top