• HABARI MPYA

  Jumatano, Julai 17, 2019

  AZAM FC KUKUTANA NA WABABE WENGINE WA DRC, MANYEMA UNION NUSU FAINALI KAGAME

  Na Mwandishi Wetu, KIGALI
  MABINGWA watetezi, Azam FC watamenyana na Manyema Union ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika Nusu Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame Ijumaa mjini Kigali Rwanda.
  Hiyo ni baada ya Manyema kuwatoa wenyeji, APR kwa penalti 4-3 kufuatia sare ya 0-0 katika Robo Fainali ya mwisho ya michuano hiyo usiku wa leo Uwanja wa Nyamirambo mjini Kigali.
  Katika Robo fainali iliyotangulia na ya tatu jioni ya leo, Green Eagles ya Zambia iliitupa nje Gor Mahia ya Kenya kwa kuichapa mabao 2-1. 

  Azam FC itamenyana na Manyema Union ya DRC katika Nusu Fainali ya Kombe la Kagame Ijumaa

  Nicholas Kipikirui alitangulia kuifungia Gor Mahia dakika ya pili na Eagles ikatoka nyuma kwa mabao ya Tapson Kaseba dakika ya nane na Shadrack Mulungwe dakika ya 69 kupata ushindi huo.
  Green Eagles yenye itakutana na KCCA katika Nusu Fainali ya pili Ijumaa pia Saa 1:30 usiku baada ya Azam FC kuanza kuumana na Manyema Union Saa 11:00 jioni Uwanja wa Nyamirambo.
  Azam FC ilitinga Nusu Fainali kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya TP Mazembe ya DRC pia jana, wakati KCCA iliwatoa wenyeji wengine, Rayon Sports kwa kuwachapa pia 2-1. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM FC KUKUTANA NA WABABE WENGINE WA DRC, MANYEMA UNION NUSU FAINALI KAGAME Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top