• HABARI MPYA

  Thursday, July 11, 2019

  SENEGAL NA NIGEIRIA ZATINGA NUSU FAINALI AFCON 2019

  TIMU za Senegal na Nigeria zimefanikiwa kwenda hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kuwatoa wapinzani wao, Benin na Afrika Kusini usiku wa Jumatano nchini Misri.
  Ilianza Senegal kuitupa nje Benin kwa kuichapa 1-0 Uwanja wa Juni 30 mjini Cairo, bao pekee la kiungo wa Everton, Idrissa Gana Gueye dakika ya 69 akimalizia pasi ya mshambuliaji wa Liverpool, Sadio Mane.
  Mane alitumbukiza mipira miwili nyavuni, lakini mara zote mabao yake yalikataliwa kwa Msaada wa Teknolojia ya Video (VAR) na Benin ikamaliza pungufu baada ya Olivier Verdon kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 82.

  Na Uwanja wa Kimataifa wa Cairo Nigeria ikaichapa 2-1 Afrika Kusini katika mchezo mwingine Robo Fainali ya michuano hiyo, mabao yake yakifungwa na kiungo wa Villarreal ya Hispania, Samuel Chimerenka Chukwueze dakika ya 27 na beki wa Udinese ya Italia, William Troost-Ekong dakika ya 89.
  Afrika Kusini ilipata bao lake la kufutia machozi kupitia kwa Bongani Zungu dakika ya 7.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SENEGAL NA NIGEIRIA ZATINGA NUSU FAINALI AFCON 2019 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top