• HABARI MPYA

  Jumamosi, Julai 13, 2019

  KMC YAWACHAPA RAYON SPORT 1-0 LAKINI WATOLEWA KOMBE LA KAGAME

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  PAMOJA na ushindi wa 1-0 katika mchezo wake wa mwisho wa Kundi A Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame timu ya KMC ya Kinondoni mjini Dar es Salaam imetupwa nje ya michuano hiyo.
  Bao pekee la kiungo mshambuliaji Hassan Salum Kabunda dakika ya 30 limeipa ushindi wa 1-0 KMC dhidi ya wenyeji, Rayon Sports Uwanja wa Nyamirambo mjini Kigali.
  Mechi nyingine za Kundi A leo TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imeichapa 6-1 Atlabara ya Sudan Kusini na Uwanja wa Nyamirambo mjini Kigali.

  Kwa matokeo hayo, TP Mazembe na Rayon Sport zimemaliza na pointi sawa, sita kila moja na kufuzu Robo Fainali kwa pamoja, huku KMC na Atlabara zikifanya safari kurejea ‘makwao’. 
  TP Mazembe na Rayon Sport zinaungana na wenyeji wengine APR, mabingwa watetezi, Azam FC ua Tanzania pia, KCCA ya Uganda na Green Eagles ya Zambia zilizotangulia Robo Fainali kutoka Kundi B na C.
  Michuano hiyo itahitimishwa kesho kwa mechi za Kundi D kati ya mabingwa wa zamani, Gor Mahia ya Kenya dhidi ya KMKM ya Zanzibar kuanzia Saa 8:00 mchana kabla ya Port ya Djibouti kukipiga na Manyema Union ya DRC kuanzia Saa 10: 30 jioni.
  Kwa sasa Gor Mahia inaongoza Kundi D ikiwa pointi zake sita, ikifuatiwa na Manyema Union ya DRC yenye pointi tatu sawa na Port, wakati KMKM inashika mkia ikiwa haina pointi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KMC YAWACHAPA RAYON SPORT 1-0 LAKINI WATOLEWA KOMBE LA KAGAME Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top