• HABARI MPYA

  Ijumaa, Julai 26, 2019

  KIINGILIO CHA CHINI TAIFA STARS NA HARAMBEE JUMAPILI NI SH 3,000 TU TAIFA

  Na Asha Said, DAR ES SALAAM  
  VIINGILIO vya mchezo wa kuwania fainali ya Kombe la Maitafa ya Afrika kwa wachezaji wa Ndani CHAN kati ya Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars na timu ya Taifa ya Kenya ni 3000 kwa jukwaa la mzunguko na VIP B na C itakuwa sh.5000.                                              
  Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira Tanzania (TFF), Cliford Ndimbo, amesema katika mchezo huo utakaochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa, tiketi zitaanza kuuzwa kesho.    
  Amesema kuwa maandalizi ya mchezo huo yamekamilika, huku wapinzani wanatarajia kuwasili nchini leo jioni.Katika kuelekea mchezo huo baadhi ya waandishi wa habari walipata nafasi ya kuzungumza na waandishi ambapo kwa niaba yao Fatma Likwata, amewataka mashabiki wa soka wajitokeze kwa wingi kuishangilia timu hiyo.

  Amesema kujitokeza kwa wingi kutasiadia kuwapa molari wachezaji wa Stars waweze kufanya vizuri katika mchezo huo muhimu.      
  'Naomba tujitokeze kwa wingi katika Uwanja wa Taifa tuweze kuwapa sapoti Stars ushirikiano waweze kuvuka hatua hii"amesema Likwata.
  Endapo Stars itashinda mechi zake zote mbili  dhidi ya Kenya itakutana na Kati ya timu ya Taifa ya Burundi au Sudan, ikishinda itakuwa imepita katika hatua ya fainali ya Michuano hiyo.       
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KIINGILIO CHA CHINI TAIFA STARS NA HARAMBEE JUMAPILI NI SH 3,000 TU TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top