• HABARI MPYA

  Ijumaa, Julai 19, 2019

  AZAM FC YAWANG’OA WAKONGO WENGNE NA KUTINGA FAINALI KOMBE LA KAGAME

  Na Mwandishi Wetu, KIGALI
  MABINGWA watetezi, Azam FC wamefanikiwa kuingia fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame baada ya ushindi wa penalti 5-4 kufuatia sare ya 0-0 ndani ya dakika 120 dhidi ya AS Manyema Union ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) leo Uwanja wa Nyamirambo mjini Kigali, Rwanda.
  Baada ya ushindi huo, Azam FC imeweka rekodi ya kuzing’oa timu zote mbili za DRC zilizoalikwa kushiriki michuano hiyo, baada ya awali kuitoa TP Mazembe katika hatua ya Robo Fainali kwa kuichapa mabao 2-1 Julai 16.
  Katika mchezo uliotangulia wa Nusu Fainali, KCCA ya Uganda iliifunga Green Eagles ya Zambia mabao 4-3 katika mchezo uliodumu kwa dakika 120 baada ya sare ya 2-2 ndani ya dakika 90.
  Wachezaji wa Azam FC wakishangilia na kocha wao, Etienne Ndayiragijje leo mjini Kigali baada ya mchezo
    
  Mabao ya KCCA itakayokutana na Azam katika fainali Jumapili yamefungwa na Allan Okello dakika ya pili na ya 80, Mike Mutyaba dakika ya 79 na Anaku Saadat dakika ya 101.
  Na mabao ya Green Eagles itakayokutana na Manyema Union katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu yamefungwa na Amity Shamende dakika ya 38 na 52 na Christopher Chola dakika ya 117.
  Ikumbukwe katika mchezo wa Kundi B, KCCA iliilaza Azam FC 1-0 Julai 9 na kumaliza kileleni huku mabingwa watetezi wakishika nafasi ya pili n azote kwenda Robo Fainali.
  Azam FC itawania kuwa timu nyingine ya Tanzania, baada ya Yanga SC mwaka 1993 na 1999 mjini Kampala, Uganda kutwaa Kombe la Kagame nje ya ardhi ya nyumbani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM FC YAWANG’OA WAKONGO WENGNE NA KUTINGA FAINALI KOMBE LA KAGAME Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top