• HABARI MPYA

  Alhamisi, Julai 18, 2019

  TAIFA STARS YAPANGWA NA TUNISIA, LIBYA NA EQUATORIAL GUINEA KUFUZU AFCON 2021

  Na Mwandishi Wetu, CAIRO
  TANZANIA imepangwa Kundi J kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika 2021 nchini Cameroon pamoja na Tunisia, Libya na Equatorial Guinea.
  Tunisia ilifungwa na Nigeria 1-0 jana katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu AFCON 2019 nchini Misri na Tanzania ilifungwa mechi zote tatu za Kundi C 2-0 na Senegal, 3-2 na Kenya na 3-0 na Algeria.
  Libya na Equatorial Guinea zote hazikufuzu fainali za AFCON mwaka huu ambazo zimeshuhudia timu za Kundi C tupu, Algeria na Senegal zikiingia fainali.
  Kenya iliyokuwa kundi moja na Tanzania kwenye fainali za mwaka huu, yenyewe kwenye mbio za Cameroon 2021 imepangwa Kundi G na Misri, Togo na Comoro na mechi za kwanza zitachezwa kati ya Novemba 7 na 11.
  Uganda wamepangwa Kundi B pamoja na Burkina Faso, Malawi na ama Sudan Kusini au Shelisheli, wakati Algeria imepangwa Kundi H pamoja na Zambia, Zimbabwe na Botswana na Senegal ipo Kundi I pamoja na Kongo, Guinea Bissau na Eswatini.

  MAKUNDI YOTE KUFUZU AFCON 2021 CAMEROON
  Kundi A: Mali, Guinea, Namibia, Liberia/Chad
  Kundi B: Burkina Faso, Uganda, Malawi, Sudan Kusini/Shelisheli
  Kundi C: Ghana, Afrika Kusini, Sudan, Mauritius/Sao Tome
  Kundi D: DRC, Gabon, Angola, Djibouti v Gambia
  Kundi E: Morocco, Mauritania, CAR, Burundi
  Kundi F: Cameroon, Cape Verde, Msumbiji, Rwanda
  Kundi G: Misri, Kenya, Togo, Comoro
  Kundi H: Algeria, Zambia, Zimbabwe, Botswana
  Kundi I: Senegal, Congo, Guinea Bissau, Eswatini
  Kundi J: Tunisia, Libya, Tanzania, Equatorial Guinea
  Kundi K: Ivory Coast, Niger, Madagascar, Ethiopia
  Kundi L: Nigeria, Benin, Sierra Leone, Lesotho
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TAIFA STARS YAPANGWA NA TUNISIA, LIBYA NA EQUATORIAL GUINEA KUFUZU AFCON 2021 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top