• HABARI MPYA

  Jumanne, Julai 23, 2019

  YANGA SC YASHINDA 7-0 MECHI ZA KUJIANDAA NA MSIMU MORO, SIBOMANA APIGA HAT- TRICK

  Na Mwandishi Wetu, MOROGORO
  TIMU ya Yanga SC imeshinda mechi ya tatu mfululizo leo katika kambi yake ya Morogoro kujiandaa na msimu upya baada ya kuichapa ATN 7-0 Uwanja wa Chuo cha Biblia, Bigwa mkoani Morogoro.
  Mshambuliaji wa kimataifa wa Rwanda, Patrick Sibomana amefunga mabao matatu peke yake, huku mengine mawili yakifungwa na nyota wa Namibia, Sadney Urikhob, Mganda Juma Balinya na beki Mghana, Lamine Moro moja kila mmoja.   
  Mechi mbili zilizotangulia Yanga ilishinda 2-0 dhidi ya Moro Kids mabao ya Balinya na beki wa kulia, Paul Godfrey ‘Boxer’ ambaye alikosekana leo kufuatia kujiunga na timu ya taifa ya Tanzania kwa maandalizi ya mchezo wa kufuzu Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) dhidi ya Kenya Jumapili.
  Patrick Sibomana akikabidhiwa mpira baada ya kufunga hat trick leo Morogoro

  Na mechi ya kwanza Yanga ilishinda 10-0, kiungo mshambuliaji, Mrisho Khalfan Ngassa akifunga mabao matatu peke yake, mengine Feisal Salum, Raphael Daudi, Mapinduzi Balama, Mkongo Papy Kabamba Tshishimbi, Wanyarwanda Patrick Sibomana, Issa Bigirimana na Balinya, 
  Yanga inajiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa Agosti 4, Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam katika kilele cha Siku ya Mwananchi dhidi ya timu ambayo itatajwa baadaye kufuatia kujitoa kwa AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
  Na yote hayo ni maandalizi ya mchezo wao wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Yanga SC wkianza na Township Rollers ya Botswana kati ya Agosti 9 na 11 mjini Dar es Salaam kabla ya kurudiana nao mjini Gaborone kati ya Agosti 23 na 25.
  Ikifanikiwa kuvuka raundi ya kwanza Yanga itakutana na mshindi kati ya Green Mamba ya Eswatini na Zesco ya Zambia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA SC YASHINDA 7-0 MECHI ZA KUJIANDAA NA MSIMU MORO, SIBOMANA APIGA HAT- TRICK Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top