• HABARI MPYA

  Jumatano, Julai 10, 2019

  SIMBA QUEENS WANAKWENDA UJERUMANI NA WACHEZAJI 13, VIONGOZI WATATU

  Na Asha Said, DAR ES SALAAM
  Na Asha Said.                   
  KIKOSI cha Simba Queens kinatarajia kuondoka nchini Jumatatu ijayo kwenda Ujerumani kwa ajili ya mwaliko wa wiki mbili.
  Simba Queens ipo katika maandalizi ya kujiweka sawa baada ya kumaliza ligi ya wanawake ikiwa nafasi ya tatu, hivyo kufanikiwa kupata nafasi ya kwenda kufanya mazoezi ya wiki mbili nchini humo.
  Mtendaji Mkuu wa Simba SC, Crescentius John Magori amesema timu yao ya wanawake imepata mwaliko kwenda Ujerumani kwa ajili ya mazoezi ya wiki mbili.

  Pamoja na hilo pia watacheza michezo minne ya kirafiki ambapo michezo mitatu itachezwa mjini Hamburg na mwingine mmoja kwenye mji mkuu wa nchi hiyo, Berlin.
  Baada ya semina ambayo itakuwa na manufaa makubwa kwa wachezaji wetu na michezo ya kirafiki ambayo itasaidia kuandaa kikosi kwa msimu ujao wa Ligi Kuu ya Wanawake, msafara wa Simba Queens utarejea nchini siku ya Alhamisi Agosti mosi, 2019.
  Safari ya Simba Queens imedhaminiwa na Serikali ya Ujerumani kwa kushirikiana na Simba SC.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA QUEENS WANAKWENDA UJERUMANI NA WACHEZAJI 13, VIONGOZI WATATU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top