• HABARI MPYA

  Alhamisi, Julai 11, 2019

  NIYONZIMA AREJEA NYUMBANI RWANDA KUMALIZIA SOKA YAKE, AJIUNGA NA AS KIGALI

  Na Mwandishi Wetu, BUKOBA
  KIUNGO wa kimataifa wa Rwanda, Haruna Niyonzima amesaini mkataba wa mwaka mmoja kurejea kwao, akijiunga na klabu ya AS Kigali.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29, baada ya miaka nane ya kucheza Tanzania akianza na klabu ya Yanga kwa miaka sita kabla ya kuhamia kwa mahasimu, Simba SC misimu miwili iliyopita, amerejea nyumbani.
  Niyonzima anakuwa mchezaji mpya wa tisa kusajiliwa na AS Kigali baada ya beki wa kulia, Michel Rusheshangoga kutoka APR, kipa wa zamani wa APR na Rayon Sports, Eric ‘Bakame’ Ndayishimiye, Rashid Kalisa kutoka SC Kiyovu na nyota wa zamani wa Marines, Christian Ishimwe pamoja na Wacameroon watatu na Mgabon mmoja.

  Wachezaji wapya wa kigeni wa AS Kigali ni Ekandjoum Essombe Arsitide (Union de Douala, Cameroon) Makon Nlogi Thierry (Coton Sport, Cameroon), Allogo Mba Rick Martel (Manga Sport, Gabon) na Fosso Fabrice Raymond (UMS de Loum, Cameroon).
  AS Kigali itakuwa klabu ya nne ya Rwanda kwa Haruna kuchezea, kwani kabla ya kwenda Ligi Kuu ya Tanzania Bara alichezea vigogo Rayon Sports na APR akitokea Etincelles.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NIYONZIMA AREJEA NYUMBANI RWANDA KUMALIZIA SOKA YAKE, AJIUNGA NA AS KIGALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top