• HABARI MPYA

  Jumatatu, Julai 15, 2019

  KASEJA AREJESHWA TAIFA STARS KUIVAA HARAMBEE KUWANIA TIKETI YA CHAN 2020

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MLINDA mlango mkongwe nchini, Juma Kaseja amerejeshwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania kwa ajili ya mchezo wa kuwania tiketi ya Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) dhidi ya Kenya Julai 27.
  Taifa Stars watakuwa wenyeji wa Harambee Stars Julai 27 katika mchezo wa kwanza Raundi ya kwanza ya mchujo wa kuwania fainali za CHAN 2020, michuano inayoshusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee kabla ya timu hizo kurudiana Agosti 2 mjini Nairobi.
  Na Kaimu kocha wa Taifa Stars, Mrundi Etienne Ndayiragijje aliyeteuliwa wiki iliyopita baada ya kuondolewa Mnigeria, Emanuel Amunike leo ametaja kikosi cha wachezaji 26 kwa ajili ya mchezo huo, akimjumuisha kipa wa klabu yake, Kaseja.

  Juma Kaseja amerejeshwa Taifa Stars kwa ajili ya mchezo wa kuwania tiketi ya Fainali za CHAN dhidi ya Kenya Julai 27

  Wachezaji walioitwa ni pamoja na makipa; Aishi Manula (Simba SC), Juma Kaseja (KMC) na Metacha Mnata (Yanga SC). 
  Mabeki; Paul Godfrey (Yanga SC), Boniphace Maganga (KMC), Gardiel Michael (Simba SC), Paul Ngalema (Namungo FC), David Mwantika (Azam FC), Iddi Mobi (Polisi Tanzania), Kelvin Yondan (Yanga SC).
  Viungo ni Erasto Nyoni (Simba SC), Jonas Mkude (Simba SC), Abdulaziz Makame (Yanga SC), Mudathir Yahya (Azam FC), Ibrahim Ajibu (Simba SC), Salum Abubakar ‘Sure Boy’ (Azam FC), Masoud Abdallah ‘Cabaye’ (Azam FC), Feisal Salum (Yanga SC), Frank Domayo (Azam FC), Hassan Dilunga (Simba SC) na Iddi Suleiman ‘Nado’ (Azam FC).
  Washambuliaji ni John Bocco (Simba SC), Ayoub Lyanga (Coastal Union), Kelvin John (Serengeti Boys), Salim Aiyee (KMC) na Shaaban Iddi Chilunda Azam FC. 
  Kikosi cha Taifa Stars inayodhaminiwa na Serengeti Breweries Limited (SBL) kitaingia kambini Julai 21 mjini Dar es Salaam, yaani wiki moja kabla ya mchezo wa kwanza.
  Pamoja na Kocha Mkuu Ndayiragijje, Wasaidizi ni Juma Mgunda wa Coastal Union, Suleiman Matola wa Polisi Tanzania na Meneja, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ wa Yanga SC.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KASEJA AREJESHWA TAIFA STARS KUIVAA HARAMBEE KUWANIA TIKETI YA CHAN 2020 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top