• HABARI MPYA

  Sunday, July 14, 2019

  NI AZAM FC NA TP MAZEMBE KATIKA ROBO FAINALI KOMBE LA KAGAME JUMANNE KIGALI

  Na Mwandishi Wetu, KIGALI
  MABINGWA watetezi, Azam FC watamenyana na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika Robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame.
  Huo utakuwa mchezo wa kwanza kabisa wa Robo Fainali na utafanyika Jumanne kwenye Uwanja wa Nyamirambo mjini Kigali, ambao utafuatiwa na mchezo kati ya KCCA ya Uganda na wenyeji, Rayon Sports.
  Robo Fainali nyingine zitafuatia Jumatano, wenyeji wengine APR wakimenyana na Manyema Union, kabla ya Gor Mahia ya Kenya kuumana na Green Eagles ya Zambia.

  Hiyo ni baada ya leo hatua ya makundi ya michuano hiyo kuhitimishwa kwa mechi za Kundi D, Gor Mahia wakiifunga 1-0 KMKM ya Zanzibar na Manyema Union ya DRC ikiifunga Port ya Djibouti 2-1 uwanja wa Umuganda mjini Gisenyi.
  Kwa matokeo hayo, Gor Mahia imeongoza Kundi D kwa pointi zake tisa, ikifuatiwa na Manyema Union ya DRC yenye pointi sita sawa, Port pointi tatu, wakati KMKM imeshika mkia ikiwa haina pointi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NI AZAM FC NA TP MAZEMBE KATIKA ROBO FAINALI KOMBE LA KAGAME JUMANNE KIGALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top