• HABARI MPYA

  Sunday, July 21, 2019

  MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA MAANDALIZI YA MSIMU MPYA WA LIGI

  Na Dominick salamba, DAR ES SALAAM
  KUMEKUWA na tambo, vijembe na dhihaka mbalimbali baina ya mashabiki wa soka huku kila mmoja akijinasibu kuwa timu yake ndio imeweka kambi ya maandalizi ya msimu katika eneo bora na kudhihaki kambi ya upande mwingine. 
  Si jambo baya maana ndiyo miongoni mwa mambo yanayoleta msisimko na kuchochea hali ya ushindani baina ya timu moja na nyingine. Hivyo nimeona nikupe kidogo mambo ya muhimu ili hata ikitokea timu yako kutofanya vizuri  uwe na uwanja mpana wa kipima na kujua kama kipindi cha maandalizi mambo ya msingi yalizingatiwa, na je kambi ilikuwa sehemu sahihi?ilipendekezwa na benchi la ufundi?vifaa muhimu vya kujifunzia vilipatikana?utulivu ulikuwepo?na mengine mengi badala ya kuanza kuangalia kambi mmenda na bajaji,bodaboda,gari au ndege.

  Kuna wakati tumeshudia timu zikianzia ufukweni,na maeneo mengine hasa waalimu wakiangalia zaidi maeneo ambayo wanatamani kuyaboresha kuzingatia ripoti ya msimu uliyopita lakini pia kuzingatia aina ya wachezaji walipo,na wale ambao wamesajiliwa uku idadi ya waliongezwa na waliopo kikiwa ni miongoni mwa vigezo muhimu katika kuangalia aina ya maandalizi ya msimu ujao. GONGA HAPA KUSOMA ZAIDI
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA MAANDALIZI YA MSIMU MPYA WA LIGI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top