• HABARI MPYA

  Alhamisi, Julai 18, 2019

  FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO, LIGI YA MABINGWA SASA MECHI MOJA TU

  SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limesema kuanzia msimu huu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho itakuwa mechi moja tu katika Uwanja maalum utakaoteuliwa.
  Hayo yamesemwa na Makamu wa Rais wa CAF, Amaju Pinnick katika taarifa yake kwa vyombo vya Habari Jumatano na kwamba maelezo zaidi yatatolewa baadaye.
  Lakini uamuzi huo umeonekana kupingwa vikali na mashabiki kwenye mitandao ya kijamii wakisema kwamba kulingana na miundombinu ya Afrika, hali ya kiuchumi no tofauti na Ulaya kuna hatari mechi hizo bila kuwa na watazamaji wengi uwanjani.

  Mechi mbili za fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu hazikukamilika baada ya Wydad Casablanca ya Morocco kugombea mchezo wa marudiano na wenyeji, Esperance mjini Tunis nchini Tunisia dakika ya 59 wakipinga maamuzi ya refa kukataa bao lao ambalo lingekuwa la kusawazisha.
  Kutokana na mechi kuvunjika, Esperance wakapewa Kombe na kutawazwa kuwa mabingwa wa Afrika , lakini uamuzi huo ulitenguliwa na Kamati ya Utendaji ya CAF iliyoagiza marudio ya mchezo huo, ingawa timu zilikata rufaa Mahakama ya Usuluhishi ya Kimichezo (CAS) kila moja ikitaka ipewe ubingwa.
  Katika hatua nyingine, idadi ya timu kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake imeonhezwa kutoka nane hadi 12.
  Na Alhamisi CAF itakuwa na mkutano mjini Misri kesho ambao pamoja na mambo mengine, utajadili kashfa ya rushwa ya inayokabili Rais wake, Ahmad.
  Mkutano huo utakaohudhuriwa na nchi 54 wanachama wa CAF utafanyika baada ya kuibuka madai dhidi ya Rais Ahmad mwezi Aprili, mwaka huu.
  Ahmad, Waziri wa zamani wa nchini mwake, Madagascar, Machi mwaka huu alishitakitiwa Kamati ya Maadili ya FIFA na Katibu wa CAF, Amr Fahmy ambaye baada ya hapo alifukuzwa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO, LIGI YA MABINGWA SASA MECHI MOJA TU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top